
Wabunge na wawakilishi kutoka chama cha mapinduzi(CCM) wamepongezana hatua ya kiongozi wa kanisa katoliki Jimbo la Dar es salaam, mwadhama Polycarp Kardinali Pengo kueleza kuwa kanisa halikutoa msimamo wake juu ya muundo wa serikali unaotakiwa.
Pia wameeleza hofu zao kuhusu uwepo wa dalili za baadhi ya vyama upinzani,kutoka vurugu mchakato wa kupatikana kwa katiba mpya. Pengo katika mkutano na waandishi wa habari juzi Dar es salaam alipinga waraka unaodaiwa kutolewa na Tume ya Haki na Amani ya Baraza la Maaskofu Tanzania(TEC) kuhusu muundo wa serikali tatu na kusema sio kanisa katoliki nchini.

No comments:
Post a Comment