Tuma picha za matukio kwa whatsup +255744268417 Kwa habari tuma kwenye e-mali maishablognews@gmail.com

Saturday, March 29, 2014

RAIS JAKAYA KIKWETE AZUNGUMZA NA MABALOZI WA NCHI ZA JUMUIYA YA ULAYA

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mkutano na Mabalozi wa nchi za Jumuiya ya Ulaya (EU) Ikulu jijini Dar es salaam leo.PICHA NA IKULU.
Chanzo, jiachie

TATIZO LA UCHAFU MANISPAA YA IRINGA LAWA SUGU

uchafu_kihesa_1_cf26d.png
Eneo la Kihesa Mtaa wa Idunda na Lugalo Manispaa ya Iringa.
uchafu_mwangata_3_19847.png
uchafu_mwangata_2_4ee56.png
Eneo la Mwangata A karibu na Kituo cha Daladala za Kidamali Manispaa ya Iringa. .(Picha na Martha Magessa)
mjengwablog.com

TATIZO LA DAWA KATIKA ZAHANATI YA NZIHI

zahanati_ya_kidamali_1b87e.png
Kituo cha Afya Nzihi Kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Vijijini Tarafa ya Kalenga.
sagi_1_89ae8.png
Waandishi wa Habari wa kwanzajamii/mjengwablog Edraw Sagini ameketi katika kiti na mwandishi mwenzake Josephin Mkude akiwa amesimama pembezoni mwa ukuta wakisubiri dawa walizo agiza baada ya kuambiwa dawa Zahanati hapo hakuna na kuamua kuagiza kwa kutoa Fedha zao mfukoni ili kuweza kupata huduma ya Kwanaza katika Zahanati ya Nzihi iliyopo Karafa ya kalenga baada ya kujisikia vibaya wakiwa kikazi Kijijini hapo.
sag_ee3cd.png
Mwandishi wa Habari wa Kwanzajamii/mjengwablog Edraw Sagini akipaiwa huduma ya kwanza na Muhudumu wa Zahanati hiyo Agatha Geka baada ya kujisikia vibaya kwa kubanwa na kifua akiwa kikazi katika kijiji cha Nzihi Tarafa ya Kalenga.(Picha na Martha Magessa)

mjengwablog.com

MANCHESTER UNITED YAICHAPA ASTON VILLA 4-1

rooney_77d6f.jpg
Wayne Rooney akishangilia baada ya kufunga goli.
Na Riziki Mashaka.
Manchester United imevunja ukimya baada ya kuitandika timu ya Aston Villa magoli 4-1 katika uwanja wake wa Old Trafford, Aston Villa walikuwa wa kwanza kupachika goli kupitia kiungo wake, Ashley Westwooh mnamo dakika ya 13 ya mchezo, wakati timu zote mbili zikifanyiana mashambulizi ya kushtukiza hali ilikuwa ni ngumu kwa upande wa Man United baada ya kuwa nyuma kwa goli 1-0, mashabiki wa timu hiyo walijawa na wasiwasi baada ya kupigwa goli la mapema.
Wayne Rooney alisawazisha goli hilo mnamo dakika ya 20 na kufikia dakika ya 44 Man United walipata goli la pili kupitia mkwaju wa penati uliowekwa wavuni na mshambuliaji huyo (Rooney), mpaka timu hizo zikienda mapumziko mashetani wekundu walikuwa kifua mbele kwa jumla ya magoli 2-1
Manchester United walilishambulia lango la Aston Villa mara mara wakati mtanange huo ulipokuwa ukiendelea katika kipindi cha pili na kufikia dakika ya 57, mhispaniola, Juan Matta alipachika goli na kuiweka kifua mbele timu hiyo kwa jumla ya magoli 3-1, vijana wa moyes walikuwa wakifanya mashambulizi ya hatari katika lango la Aston Villa katika kipindi cha pili.
Javi Hernandez (Chicharito), aliyetokea benchi aliifungia goli Man United mnamo dakika ya 90 na kuiweka kifua mbele timu hiyo kwa jumla ya magoli 4-1, kwa matokeo hayo timu ya Manchester United imefikisha jumla ya pointi 54 na kuendelea kubaki katika nafasi ya 7 kwenye msimamo wa ligi hiyo.
moyes_89c07.jpg
Kocha wa timu hiyo (David Moyes) 
Akiongea na skysports Tv, kocha wa timu hiyo (David Moyes) amesema amefurahishwa na kiwango kilichooneshwa na vijana wake na kusisitiza kuwa bado watapigana mpaka hatua ya mwisho ya ligi hiyo.

PINDA KUKUTANA NA SURPRISE LEO DODOMA

Untitled
WAZIRI Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda leo atakutana na 'surprise' ya aina yake, wakati atakapokabidhi tuzo kwa mwanamke bora wa mwaka, ambaye hadi sasa bado hajafahamika ni nani kati ya wanawake wanne mahiri nchini, itakayofanyika katika Ukumbi wa The African Dream, Dodoma.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ndiye atakuwa mgeni rasmi katika utoaji tuzo.
Wanawake hao ambao mmoja wao ataibuka kinara na kuondoka na Tuzo na zawadi maalum ni pamoja na Dk. Maria Kam, Dk. Asha Rose Migiro, Profesa Anna Tibaijuka na Mheshimiwa Anna Kilango Malecela ambao wamefikia hatua hiyo ya mwisho baada ya kuwashinda wenzao 150 walioanza kupigiwa nao kura.
Dk. Asha Rose Migiro.
Akizungumza mjini Dar es Salaam jana, Meneja Mkuu wa Global Publishers iliyoratibu zoezi hilo, Abdallah Mrisho, waliamua kutoa tuzo hizo hasa baada ya kupata msukumo uliotokana na kuthamini michango ya wanawake nchini.
Alisema wadau hao walituma majina zaidi ya 30,000, lakini kamati iliyachuja kulingana na sifa za kila mmoja na kupata wanawake 150 ambao walianza kupigiwa kura kwa awamu. Awamu ya kwanza iliyochukua miezi miwili, iliwapata wanawake 20, iliyofuata iliwapata watano na ya mwisho iliwapata washindi hao wanne.
Prof. Anna Tibaijuka.
Mrisho alisema hafla hiyo itawahusisha waalikwa pekee ambao aliwataja kuwa ni pamoja na waheshimiwa wabunge wa bunge maalum la Katiba, wanaharakati na wawakilishi wa taasisi mbalimbali walioko mjini Dodoma kwa sasa.
Dk. Maria Kamm.
"Ikumbukwe kwamba washiriki hawa wote ni washindi, kila mmoja atapata tuzo, isipokuwa ile ya mshindi kidogo itakuwa tofauti na nyingine na zaidi, yeye atapata na zawadi nyingine," alisema
Mh. Anne Kilango Malechela.
Mrisho alisema baada ya kutolewa kwa tuzo hizo mwaka huu, mara moja wataanza mchakato wa kumpata mwanamke mwingine kwa mwaka ujao.
Aidha, katika upande wa burudani, Mrisho alisema atakuwepo msanii anayepiga nyimbo za Kiafrika, Zaid na wasanii wengine wa Bongo Fleva.
Chanzo, dejwiblog

Friday, March 28, 2014

Kurasa za mwanzo na mwisho za magazeti leo March 29 2014


.
.

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
mg7-w480-h580
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

RIDHIWANI KIKWETE AFUNIKA KATA YA PERA CHALINZE



    1
Mgombea ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia chama cha Mapinduzi Ndugu Ridhiwani Kikwete akiwahutubia wananchi katika viwanja vya kwa Mwarabu kata ya Pera Chalinze leo wakati wa mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo hilo, Unaotarajiwa kufanyika Aprili 6 mwaka huu jimboni humo, Ridhiwani amewaomba wananchi hao kumpa kura za ndiyo ifikapo Aprili 6 ili aweze kuwatumikia na kuleta maendeleo ya jimbo hilo akishirikiana na wananchi kwa ujumla wake uchaguzi huo unafanyika kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo marehemu Said Ramadhan Bwanamdogo. (PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-CHALINZE)
2
Mgombea ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia chama cha Mapinduzi Ndugu Ridhiwani Kikwete akipunga mkono juu huku Mzee Kazidi ambaye ni Katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro na Meneja wa Kampeni wa mgombea huyo akicheza wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo kwenye kata ya Pera.3
Bw. Imani Madega aliyekuwa mmmoja wa wagombea walioshiriki katika hatua za awali za mchujo ndani ya Chama cha Mapinduzi akimuombea kura Ridhiwani Kikwete wakati wa mkutano huo wa kampeni.
4
Mgombea ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia chama cha Mapinduzi Ndugu Ridhiwani Kikwete na msafara wake wakiondoka katika kijiji cha Pingo Kata ya Pera mara baada ya kumaliza mkutano wa kampeni kijijini hapo.(P.T)
5
Mgombea ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia chama cha Mapinduzi Ndugu Ridhiwani Kikwete akihutubia mkutano wa kampeni katika kijiji cha Pingo kata ya Pera leo.
7
Umati wa wananchi waliohudhuria katika mkutano uliofanyika kata ya Pera.
9
Umati wa wananchi waliohudhuria katika mkutano uliofanyika kata ya Pera.
10
Mgombea ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia chama cha Mapinduzi Ndugu Ridhiwani Kikwete akicheza na wakina mama kabla ya kuanza kwa mkutano huo.
11
Mgombea ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia chama cha Mapinduzi Ndugu Ridhiwani Kikwete akicheza na Mwanamuziki Hafsa Kazinja
12
wananchi wakifurahia wakati Hafsa Kazinja alipokuwa akitumbuiza katika mkutano huo.
14
Ridhiwani Kikwete akisalimiana na viongozi wa Dini na baadhi ya wazee wa Chalinze wakati alipowasili katika mkutano huo wa kampeni uliofanyika kata ya Pera leo.
15
Burudani zikiendelea
16
Sam wa Ukweli akiburudisha katika mkutano huo.
17
Ridhiwani Kikwete akisalimiana na Baadhi ya wazee wa Kimasai wakati alipowasili katika kijiji cha Chamakwera Kata ya Pera na kufanya mkutano wa kampeni katika kijiji hicho.

mjengwablog.com