Tuma picha za matukio kwa whatsup +255744268417 Kwa habari tuma kwenye e-mali maishablognews@gmail.com

Monday, March 3, 2014

FRANCIS MIYEYUSHO: USWAZI KUNAHARIBU WANAMICHEZO


miyeyusho_64467.jpg
Kutokana na mchezo wa ngumi kuonekana kuwa mgumu na kuhitaji watu wakakamavu, wenye
Katika Jiji la Dar es Salam maeneo kama Tandale, Temeke, Magomeni, Manzese, Keko, Kinondoni ni baadhi ya maeneo yenye sifa hizo. Maeneo ya Morogoro na baadhi ya sehemu za Mkoa wa Mbeya nazo zimesheheni sifa hizo.
Katika hali isiyo ya kawaida mabondia wanaofanya vizuri na kujizolea umaarufu nchini wamekuwa wakitokea kwenye maeneo hayo ya uswazi, hii inawezekana inachangiwa na aina ya mchezo.
Mchezo huo wa ndondi huhitaji watu wakakamavu, wenye stamina na uvumilivu ambao ni vigumu sana kuwapata maeneo ya 'Kishua' kama Mbezi Beach, Mikocheni na Masaki.
Kauli ya Miyeyusho kuhusu bangi
Alipoulizwa kuhusu shutuma kuwa mabondia wengi wanajihusisha na uvutaji wa bangi, Bondia Francus Miyeyusho alisema, "Unajua mabondia wengi tunatokea uswahilini ambako hayo mambo ndio yanafanyika. Ndiyo maana utakuta baadhi ya mabondia wanatumia vitu hivyo."
"Hili siyo la mabondia tu ila hata wanaocheza michezo mingine kama soka, riadha na kikapu wanaotokea maeneo yetu haya ya uswahilini utakuta wanatumia." Aliongeza Miyeyusho anayeishi Kinondoni Mkwajuni jijini Dar es Salaam.
Miyeyusho anadai kuwa malengo ya kutumia vitu hivyo yanatofautiana, ambapo wengine hutumia kama starehe wakati wengine hutumia ili iwasaidie kupata hamasa ya mchezo.
Mkali wa 'Knockout'
Katika mapambano 47 aliyopigana Miyeyusho, 32 yalimalizika kwa 'knockout'. Kati ya mapambano hayo 32, mapambano 23 alishinda kwa knockout na kupoteza tisa kwa knockout akiwa ndio bondia pekee wa Tanzania mwenye rekodi ya kushinda michezo mingi kwa 'knockout' na kushindwa mingi kwa staili hiyo hiyo. Katika michezo kumi aliyopoteza tisa amepoteza kwa 'knockout'
"Mimi huwa napenda kuimaliza michezo yangu kwa 'knockout' kwa sababu mara nyingi ushindi wa pointi humalizika kwa utata. Wengine huona kama bondia amependelewa ushindi kitu ambacho siyo sahihi."
"Nimepoteza mapambano mengi kwa 'knockout' kwa sababu ya kuwa na maandalizi duni, kutokana na hali ndogo ya kipato likitokea pambano hata kama sina mazoezi huwa nakubali ili nipate fedha japo ninajua sitaweza kushinda.

No comments:

Post a Comment